Saturday, 26 March 2016

FASIHI ANDISHI; Muundo na mtindo katika Tamthilia

Tamthilia hutofautiana na riwaya na hadithi fupi kutokana na muundo wake. Tamthilia hutegemea mazungumzo na uwasilishaji wa jukwaani kuupitisha ujumbe wake. Mwandishi wa tamthilia, tofauti na wengine, analazimika kuwazia:
  •  uigizaji
  • matumizi ya maleba
  • matumizi ya taa na mwangaza
  • sauti za wahusika au vifaa vingine
  • matumizi ya kimya
  • ngoma na uchezaji
  • kuwepo kwa wahusika mbele ya hadhira na jukwaa lenyewe.
Tamthilia huwa na kaida au kanuni maalum ambazo hazipatikani katika tanzu nyingine za kifasihi. kanuni hizi zinahusiana na:
  • matumizi ya usemaji kando
  • ugawaji wa sehemu mbalimbali kwenye maonyesho au matendo
  • matumizi ya mbinu ya ujifanyaji- mhusika mmoja anapojifanya kuwa mhusika mwingine
  • matumizi ya mkarara au kipokeo kinachorudiwarudiwa
  • wahusika wanaojizungumzia wao
  • wahusika kuwasiliana na hadhira
  • matumizi ya ngoma, nyimbo na uimbaji kuongeza uzito.

No comments:

Post a Comment